Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika ziara hiyo ya kidiplomasia, Balozi Tkachenko alisaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika ubalozi huo kwa heshima ya kiongozi huyo wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Pia alitoa ujumbe wa pole kwa serikali na wananchi wa Iran, huku akieleza masikitiko na huzuni yake kuhusiana na tukio hilo.
Ubalozi wa Iran mjini Nairobi umeendelea kupokea viongozi wa kidiplomasia, wawakilishi wa mashirika mbalimbali na marafiki wa Iran wanaofika kutoa pole na kuonesha mshikamano wao katika kipindi hiki cha maombolezo.
Ayatullah Ali Khamenei, ambaye aliiongoza Iran kwa zaidi ya miongo mitatu, aliuawa kishahidi tarehe 28 Februari 2026 baada ya mashambulizi ya anga yaliyolenga viongozi wa juu wa Iran katika mji mkuu wa Tehran. Serikali ya Iran ilithibitisha kifo chake siku chache baadaye na kutangaza kipindi cha maombolezo kitaifa.
Kifo chake kimeibua hisia na majibu mbalimbali kutoka katika mataifa mbali mbali duniani, huku viongozi na wanadiplomasia kutoka nchi tofauti wakituma au kufikisha ujumbe wa rambirambi katika serikali ya Iran.
Maoni yako